Saturday, June 28, 2014

VYOMBO VYA HABARI VYA KIJAMII - Toeni elimu kwa jamii madhara ya unyanyasaji kijinsia Na Gladness Hemedi Munuo Vyombo vya habari vya kijamii (Community Media) vikitumika sawasawa katika kutoa habari vitajenga na kuwa msaada mkubwa wa maendeleo kwa jamii katika kuelimisha madhara yanayokuwa kwa kasi sana ambayo ni unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake, watoto na wazee. Zipo jamii nyingi sana Afrika na hususan Tanzania ambazo mila na desturi huwageuza wanawake kuwa ni viumbe duni visivyo na sauti na hata kutofaa kustahili kuwa na haki. Na wahanga wakubwa wa mila na desturi zenye mfumo dume ni wanawake na watoto ambao kukandamizwa kwao kunatafsiriwa kama ni jambo la kawaida kwa jamii. Mikataba mbalimbali ya kimataifa na kikanda ambayo nchi ya Tanzania kupitia bunge letu tukufu imeridhia, imeeleza kwa undani kuhusu uwajibikaji wa jamii na taifa kwa ujumla katika kuhakikisha kuwa mwanamke na mtoto analindwa na kuheshimiwa kama ilivyo kwa mwanaume. Hivi karibuni katika mkutano mkuu wa kwanza na kongamano kwa vyombo vya habari vya kijamii (Redio za jamii) uliofanyika mjini Bagamoyo, mambo mbalimbali yalijadiliwa katika kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vya kijamii vinaimarika na kuwa msaada muhimu kwa jamii iliyovizunguka hasa katika kuelimisha kuutoko,eza unyanyasaji. Naweza kusema kuwa, kwa jinsi kasi ya manyanyaso, uonevu na ukatili kwa wanawake na watoto unavyopamba moto siku hadi siku, wapo wataalamu mbalimbali waliotoa ari kuwa vyombo vya habari vya kijamii viwe ndiyo nguzo kubwa katika kutoa elimu kwa jamii, kwa kuwa mpaka sasa ndivyo vyombo vinavyofanya kazi kwa niaba ya jamii na karibu na jamii (Cabrella-Balleza,M.’Community media by and for women’;AMARC women’s International Network, 2007). Majadiliano hayo yalilenga katika kuona kuwa vyombo hivi ambavyo kwa ujumla takribani kwa idadi vipo zaidi ya vyombo 20 walihudhuria kongamano hilo, walitoa ari kwa vyombo hivyo viwe na manufaa kwa asilimia 100 kwa wana jamii, ikiwa ni msaada katika kuondoa kero zilizopo pamoja na kuelimisha na kuburudisha. Suala moja wapo lililowekewa mkazo ni kuhakikisha kuwa vipindi vyote vya redio viandaliwe katika mfumo wa kuhakikisha vinakidhi matakwa ya jamii zote na zaidi wanawake na watoto ili kwenda sawa na ‘Protokali ya Jinsia na Maendeleo katika kanda ya kusini mwa Afrika’. Ambayo katika kifungu cha 29-31kinazungumzia masuala ya habari, taarifa na mawasiliano na msisitizo ni kuwa ifikapo mwaka 2015 masuala ya jinsia katika vyombo vya habari yatakuwa yameshika kasi nzuri kutokana na mafunzo mbalimbali yanayotolewa kwa waandishi wa habari, aidha sera za jinsia zitaendelea kuwepo na kuhamasisha waandishi katika kutetea masuala ya jinsia. Sio jambo geni kwetu tunaposikia taarifa mbalimbali kupitia vyombo vya habari zikituhabarisha matukio ya unyanyasaji kwa wanawake na watoto yanavyokuwa siku hadi siku, na ndiyo maana msisitizo umetolewa katika kuhakikisha vyombo vya habari vya kijamii kuweka agenda ya mkakati wa kutoa elimu hii kwa umma. Katika kongamano la kwanza kwa vyombo vya habari vya kijamii, kero za unyanyasaji wa jinsia kwa jamii ilionekana kushika kasi hasa kutokana na takwimu sahihi kama zinavyoainishwa na ‘Tanzania Demographic and Health Survey (TDHS)’ ya mwaka 2010. TDHS inaonyesha kuwa unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto wa kike ambao hawana ndoa ni asilimia 44% wakati wanawake walio katika ndoa ni asilimia 20. Ikumbukwe kuwa hizi ni takwimu kwa matukio yaliyotolewa taarifa katika vituo vya polisi na mahospitalini, na penginewe ni sehemu za mijini tu. Kwa maana kwamba zipo taarifa nyingi za matukio kama hayo katika maeneo ya vijijini na zaidi ambazo hazijajulikana. Hii ni kutokana na wana familia na jamii kuamua kuyafumbia macho matatizo kama hayo na kuyageuza kama jambo la kawaida katika familia. Katika kuchangia mada hii, mwakilishi kutoka katika Redio ya Jamii Kigoma, alielezea masikitiko yake kuhusiana na haki ya watoto kielimu inavyoporomoka kiasi kusababisha watoto wa kike kukosa elimu kwa kupata ujauzito wakiwa mashuleni. Naye mshauri wa redio/vyombo vya habari vya kijamii kutoka UNESCO Bi Rose Haji alielezea umuhimu wa sera za jinsia na vyombo vya habari zinavyopaswa kufanyiwa kazi kwa vitendo, ikiwa ni pamoja na uandaaji wa vipindi, muda wa kurusha vipindi hewani kulingana na ratiba au desturi za kila siku za jamii husika. Jambo lililopongezwa katika kuhakikisha kuwa itakuwa ni rahisi kwa habari lengwa kufika kwa walengwa bila pingamizi, ni kuwepo kwa matumizi ya lugha ya Kiswahili ambayo mpaka sasa imani kubwa ni kuwa watanzania walio wengi lugha hii wanaifahamu na hasa kwa kusikia na kuelewa hata kama hawatazungumza. Hivyo basi, wito ulitolewa kwa wanahabari wa vyombo vya kijamii kutumia vyombo vya habari ikiwa pamoja na kalamu zao kama vitendea kazi katika kuhakikisha kuwa jamii inatambua madhara ya unyanyasaji yaliyopo kwa upande wa wanawake na watoto. Washiriki na wajumbe katika kongamano hilo walijadili kwa kina ya kuwa njia nzuri ya kufikisha ujumbe kwa walengwa (wasikilizaji) ni kuwepo kwa hatua za awali katika kuhakikisha hilo linatekelezeka kwa kuwajengea uwezo waandaaji na wapelekaji wa habari hizo kwa jamii kupitia vyombo vya habari vya jamii. Elimu kama hii imekuwa ikitolewa na asasi kama vile Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Asasi ya Jinsia na Maendeleo ya Vyombo vya Habari Tawi la Tanzania (GEMSAT), Baraza la Habari Tanzania (MCT) nchini na vimekuwa mara zote vikiwalenga zaidi waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya kawaida na kuwasahau waandishi waliopo katika vyombo vya habari vya kijamii. Kongamano hilo ambalo liliendeshwa kwa siku tatu, lilionyesha imani kubwa kuwa, vyombo vya habari vya kijamii vikiwezeshwa kisawasawa, basi litakuwa daraja muhimu katika kuirekebisha jamii au kuondoa kabisa kero za unyanyasaji wa kijinsia kwa jamii. Ukitaka kujua ni kwa vipi wanawake na watoto wananyanyasika kijinsia, tembelea katika vituo vya polisi vilivyopo katika maeneo ya makazi ya watu. Aidha pita katika hospitali na vituo vya afya upate kujionea visa mkasa na madhila yanawapata wanawake walio wengi. Aidha mila nyingi za jamii mbalimbali nchini Tanzania zinaongeza a na kuona kama ni sehemu ya maisha na mwanamke hana sauti ya kujitetea. Aidha, wapo wale wanaodhani kuwa, desturi ya ukandamizaji na uonevu kwa jinsia isiyo na sauti (wanawake) ni jambo sahihi au suala la kawaida. Wito umetolewa kwa wamiliki wa vyombo vya habari vya kijamii kuvalia njuga elimu ya kukomesha unyanyasaji kwa wanawake na watoto. Suala hili likitiliwa mkazo mafanikio yataonekana. Tushike maneno ambayo Hayati baba wa taifa hili muasisi wa serikali yetu na Rais wa kwanza wa Tanzania Mheshimiwa Julius Kambarage Nyerere, ambaye aliwahi kusema kuwa ‘inawezekana ikiwa kila mmoja atatimiza wajibu wake’. Gladness H. Munuo: Ni Mratibu wa Asasi ya GEMSAT Mobile No.+255 754 285701
TOGETHER WE CAN: Dar es Salaam hosts first SADC Gender Protocol Summit  Maternal Health project by CSSC became an overall winner Country and Regional wise By Gladness Hemedi Munuo Gender Links (GL) in Collaboration with Gender and Media Southern Africa Tanzania Network (GEMSAT) on March 27, 2013 hosted the first ever SADC Gender Protocol Summit at Dar es Salaam’s Blue Pearl Hotel in Tanzania. This Summit sought to comment and encourage local level initatives towards achieving the 28 targets of the SADC Gender and Development Protocol, which Tanzania has recentlry ratified. In her opening remarks, Deputy Minister for Community Development, Gender and Children, Ummy Mwalimu said that the Tanzania government aligns itself with SADC Gender and Development Protocol to achieve gender equality. Mwalimu assured stakeholders and participants that government will work closely with the media and civil society to promote gender equality in the country because ‘togethe we can’. The summit accompanied together with the provision of different Awards to various entrants to recognise the efforts made by organisations, media houses and journalists to push the gender agenda and create awareness about women’s issues and gender equality. With light blue sweater she is speaking with the community is Ms. Rache Mkunduai, a Public Relation Officer with CSSC trying to educated people on what is ‘Kangaroo Style’ and its advantages. As per this information, GEMSAT member of the Board congatulate Ms. Rachel Mkundai, Public Relations Officer of Christian Social Services Commission (CSSC) was commended and awarded in country and SADC Regional wise for the organisations contribution towards the achievement of gender equality through reproductive and maternal health “I am happy to have worked with GEMSAT and other organisations” she said so. A mother delivered premature in a Kangaroo Style of carering at one of the Health Center after CSSC introduced the practice.(All photos by CSSC) Rachel presented on a success story on how they educat3 majority rural area on how to care on premature babies by using ‘Kangaroo style’ and its success in most parties they intriduced in Tanzania. Therefore, CSSC has done such a recommendable job on that. All in all, the summit intends to mobilise media houses, journalists and civil society to unite and fight for gender equality. GL with GEMSAT is currently working with ten media houses in Tanzania, who have committed to mainstreaming gender in institutional practices and content. The summit awards rewarded journalists and media organisations who are at the forefront of gender reporting.
MIGOGORO NA VURUGU HUIBUA UNYANYASAJI KIJINSIA KWA WANAWAKE • Azimio la Umoja wa Mataifa no.1325 lilete mabadiliko Tanzania • Mabaraza ya Usalama kwa Vijiji, Kata, Wilaya na Mkoa washirikishe Wanawake Na Gladness Hemedi Munuo Imefika wakati wa nchi yetu Tanzania kupitia bunge letu tukufu kuridhia Azimio la Umoja wa Mataifa ya 1325 (UN Resolution 1325) ili kukomesha vitendo vya kikatili na unyanyasaji kijinsia wanavyotendewa wananchi wasiokuwa na hatia na hasa wanawake katika maeneo yenye migogoro. Hii ni kwa kuwa, nchi zote zilizo katika Umoja wa Afrika Mashariki tayari zilikwisha ridhia Azimio hili la Umoja wa Mataifa na utekelezaji wake ili kukidhi haja za jamii zao. Iweje Tanzania mpaka leo tunasusua wakati tayari migogoro, vita na mashambulizi ya aina mbalimbali kwa jamii hivi sasa yameshamiri. Uhalisia kamili umethibitisha kuwa, mahali popote panapotokea mgogoro, baina ya jamii kwa kutokuelewana kiasi cha kuzuka mapigano na uharibifu wa mali, vitendo vya unyanyasaji kijinsia vinavyojitokeza kama vile ubakaji kwa wanawake na watoto, utekaji nyara wa watoto wa kiume na wasichana ili waweze kuwatumikia watekaji kama watumwa au wake zao, pamoja na jamii hasa wanawake kuachwa wakiwa walemavu au kuharibiwa baadhi ya viungo vyao. Azimio la Umoja wa Mataifa la 1325, linapinga kuwepo kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha kuwa wanawake wanahusishwa katika ngazi zote za maamuzi kuhusiana na kupatikana kwa amani nchini na duniani. Vyombo vya habari vimekuwa vikijitahadi kuhabarisha umma kuhusu matukio dhalimu kama haya, lakini kwa uhakika wanao/walioathirika na majanga kama haya ni wengi, na kwa kuwa vyombo vya habari ni vichache vinavyoweza kufika vijijini na hasa maeneo yenye migogoro ili kuibua na kuhabarisha umma kikamilifu vitendo vya unyanyasaji kijinsia kwa jamii na hasa wanawake si rahisi habari nyingi kufika katika vyombo vya usalama kwa haraka. Upo msemo unaosema ‘wapiganapo tembo nyasi ndizo zinazoumia’, pamoja na ‘Vita vya Panzi ni furaha kwa Kunguru’. Misemo hii inaashiria kuwa, wakati wowote tusikiapo ya kuwa kuna mgogoro wa aina fulani kiasi kupelekea jamii kukimbia makazi yao, wazee na wagonjwa huachwa bila ya msaada wowote aidha, wapo wakina mama wanaojifungulia maporini maeneo ambayo hayana usalama kiafya ikiwa ni pamoja na wanawake kufanyiwa vitendo vya kikatili kama vile kubakwa, kulawitiwa nk. Hivyo basi, muarobaini wa athari hizi, ni kuwepo kwa maridhiano ya Azimio la Umoja wa Mataifa no.1325, ili utekelezaji wake uanze mara moja, huenda dawa ya kutokomeza migogoro hii ikiwa ni pamoja na kutibu itakuwa imekamilika kwa njia hii. Asasi ya Wanawake katika mapambano ya amani Tanzania (TAWOPE), ni moja wapo ya taasisi yenye malengo ya kuhakikisha kuwa, jamii na wanawake waliopo katika maeneo yenye migogoro wanapatiwa elimu mbalimbali kama vile kujilinda na jinsi ya kujikinga miili yao kufuatia kuzuka kwa migogoro na vurugu za mara kwa mara, ufahamu wa sheria ya ardhi vijijini ya mwaka 1999 na elimu nyingine mbalimbali. Mbali na TAWOPE, aidha zipo asasi ambazo zimejikita katika kutoa misaada mbalimbali kwa waathirika wa migogoro ya aina yeyote ile, ikiwa ni pamoja na ushauri nasaha kwa walioathirika kwa njia moja au nyingine, hizi ni asasi kama Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania (TAWLA), Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), na wengineo wengi. Aidha, zipo asasi zinazotakiwa kuwa mstari wa mbele katika kushughulikia waathirika wa migogoro hiyo kama vile waliobakwa na kupata majeraha, ujauzito na hata maradhi mbalimbali ikiwemo UKIMWI, hawa huhitajika kupata msaada wa kiafya kutoka asasi husika kama vile Chama cha Madaktari wa Kike Tanzania (MEWATA), pamoja na asasi zenye kutoa huduma kama hizo. Aidha, katika utafiti uliofanywa na TAWOPE (2010), ilionyesha kuwa katika nchi ya Tanzania maeneo ambayo kwa hakika migogoro isiyokwisha hujitokeza mara kwa mara, ni maeneo wanayoishi wafugaji na wakulima, na kikubwa hasa ni kwa wafugaji kuwa na idadi kubwa ya mifugo ambapo mara zote huingiza mifugo kwenye mashamba ya wakulima na kusababisha kuzua kutokuelewana kati yao na wakulima. Ingawaje maamuzi ya UN ya 1325 yanalenga kulinda na kutetea maslahi ya wanawake hasa katika maeneo ambayo migogoro au vurugu zenye matumizi ya silaha zimejitokeza upande mmoja au pande zote. Siyo siri kuwa, hata Tanzania, wananchi walio wengi wameshuhudia baadhi ya wafugaji wakitumia silaha ikiwa ni pamoja na bunduki zenye risasi za moto, ambazo madhara yake ni makubwa kwa jamii yote na hasa kwa wanawake ambao wamekuwa ndiyo kichaka cha uonevu. Je, mpaka leo tujiulize, Tanzania tunasubiri nini mpaka Azimio hili litupite? Vurugu au migogoro ya hivi karibuni jamii imeweza kushuhudia wakati wa Operesheni mbili za kitaifa (Tokomeza na Kimbunga), kumekuwa na vitendo vya ubakaji na kila aina ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wanaume waliokumbwa katika hizo operesheni ambazo ziligeuka na kuwa ni vurugu kwa jamii husika. Mfano halisi wa wanawake walioathirika ni pale ambapo baadhi yao wamelazimika kuolewa kinguvu na wafugaji au askari wanaosimamia operesheni mbalimbali kama tulivyoshuhudia nchini Tanzania hivi karibuni. Taarifa kama hizi zinasimuliwa na waathirika wenyewe katika maeneo ya Mahenge –Itete, Morogoro- Mvomero, Loliondo na Manyara. Aidha, Mara-Tarime, Pwani –Rufiji pamoja na maeneo mengine ambayo wafugaji wameingia kwa wingi. Angalizo pia tunatoa kwa serikali yetu, katika kipindi hiki ambacho wananchi wanajiandaa na uchaguzi wa taifa, zipo dalili ya kujitoza kwa vurugu za kisiasa ambazo kwa Tanzania tumeshashuhudia baadhi ya vifo mfano mauaji ya mwandisha wa habari huko Iringa, aidha vurugu za silaha za moto (bomu) kwa raia wasiokuwa na hatia katika nyumba za ibada Zanzibar na Arusha, na hata katika mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa.. Kipindi hiki Tanzania inapoandaa Katiba Mpya, ndiyo wakati muafaka wa kuhakikisha pia Azimio la Umoja wa Mataifa no.1325 linazingatiwa kwa kuridhia na kuhalalisha utekelezaji wake ili migogoro iliyopo na inayoendelea kujitokeza iweze kudhibitiwa. Hivyo basi, mapambano dhidi ya vitendo vya unyanyasaji kijinsia yanahitaji ushirikiano kutoka serikalini, asasi zote zenye kuunga mkono haki za binadamu pamoja na vyombo vya habari katika kuhabarisha jamii. • Mwandishi Gladness Munuo ni Mratibu wa Asasi ya Jinsia na Vyombo vya Habari, Tawi la Tanzania. 0754/0786/0754 285701