Monday, January 16, 2017

UKATILI WA KIJINSIA


 

Na Dominica Cassian Haule

Ukatili wa kijinsia ni msemo mpana sana. Unagusa binadamu wote wanawake na wanaume. Lakini ni ukweli usiopingika kwamba ukatili wa kijinsia unawaathiri kwa asilimia kubwa wanawake na wasichana kuliko ilivyo kwa wanaume na wavulana. Kuna tafiti lukuki zinazothibitisha.

Wakati wa mababu na mabibi zetu, tulisikia mwanamke kapigwa, kavunjwa mkono, kauawa na kadhalika na kadhalika. Tuliongozwa na tamaduni na kuona maisha ndivyo yanavyotakiwa kuwa.
Raia yenye furaha ni hazina kwa taifa

URITHI

Binafsi, nashawishika kuamini kuwa, ukatili wa kijinsia, umekuwepo tokea mwanzo wa uzao wa binadamu. Ukipitia maandiko mbali mbali, utakuta maandiko, mtu na mkewe. Kwa hili mimi na wewe hatuna budi kujiuliza,  hivi mtu ni nani?. 

 Lakini pia katika maandiko hay ohayo, utakutana na semi binadamu wote. Basi, na tubadilike, tukijua kuwa kwa kuwa neno binadamu wote inamaanisha watu, kwa hiyo, watu hao ni wanawake na wanaume.

Katika familia zetu, kilio kikubwa bado kinaumiza mabinti pale ambapo wazazi/walezi wanapogawa majukumu fulani kuwa ya wasichana na mengine kuwa ya wavulana. Mara nyingi inasahaulika kuwa, vyovyote iwavyo, majukumu ya wasichana yanaweza kuchukua asilimia kubwa ikilinganishwa na asilimia ya majukumu ya wavulana.

Japo kwa asilimia fulani, wakazi wa mijini wameweza kutambua umuhimu wa kuwapa watoto wao majukumu yanayofanana ili mradi hayavuki mipaka. Hii ni njia mojawapo ya kutoa malezi endelevu kwa watoto wote wa kike na wa kiume.

Kadhalika tumeshuhudia, wazazi wanaojadili kutegemea uzao wa watoto wa kiume tu. Na haya yanapatiwa baraka na wanawake pia. Fikiria mama mjamzito  anapolazimika kuomba ajaliwe mtoto wa kiume.Lakini sio kwa matashi yake, bali kwa matashi ya jamii inayomzunguka. Imemtengenezea mtizamo wa kuthamini mtoto wa kiume japoku yeye ni mwanamke.

 HABARI SAHIHI

Vyombo vya habari kwa ujumla wake navyo vinachangia kwa kasi kuwanyima uelewa mpana wananchi ili waachane na vitendo vinavyochangia ukatili wa kijinsia. Haviandiki au kutangaza kwa undani yale yanayopinga ukatili wa kijinsia, ili wananchi wapate upembuzi yakinifu.

Kwa mujibu wa jarida, Jinsia na Vyombo vya Habari Tanzania, lililobeba stadi juu ya mwendelezo wa jinsia na vyombo vya habari  (2010), sauti za wanawake zinasikika pale tu habari inapohusu ukatili wa kijinsia na usawa wa kijinsia. Ambazo zinachukua asilimia 71 na 67. Na habari hizo ni zile za udhalilishaji, mfano ukahaba, mauaji ambayo yametendwa na mwanamke na kadhalika.

 Ingefurahisha na kupongezwa iwapo habari hizo zingekuwa zile zinazoleta maendeleo kwa nchi, ukizingatia kwamba asilimia 70 – 75 ya kazi za uzalishaji hasa sehemu za vijijini hufanywa na wanawake.

La kusikitisha, habari zinazohusu madini kwa mujibu wa jarida hilo hazikupata nafasi katika vyombo vyetu vya habari. Sambamba na hizo, zile zinazohusu  ajira zilipata fursa kwa asilimia kumi tu na zile zinazohusu makazi  zilipatiwa nafasi kwa asilimia kumi kadhalika.

Stadi juu ya mwendelezo wa jinsia na vyombo vya habari Tanzania iliyoratibiwa na asasi isiyo ya kiserikali ya Jinsia na Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania – GEMSAT kwa ufadhili wa asasi isiyo ya kiserikali yenye makao makuu nchini Afrika kusini –‘ Gender Links’, imebaini pia kwamba asilimia sita (6) ya wanawake hubeba utambuzi wa mama, mke au binti kwa upande wa chanzo cha habari. Wakati asilimia nne tu (4) ya wanaume hubeba utambuzi wa baba, mtoto wa kiume au mume.

Hili lina maana gani kwetu. Ni kwamba, mwanamke au msichana  bado anatambuliwa kupitia kwa baba yake mazazi/mlezi au kupitia kwa mumewe.

Japokuwa ukatili wa kijinsia umebainika kufanyika kwa kiwango cha kutisha si tu nchini Tanzania, bali hata katika nchini zilizopo kusimwa mwa Afrika, ni asilimia tatu tu (3) ya habari zinazoandikwa na kutangwa zinaongelea ukatili wa kijinsia.

HISTORIA

Kwa mujibu wa kitabu WANAWAKE WA TANU (Jinsia na Utamaduni katika Kujenga Uzalendo Tanganyika: 1955 – 1965),”wanawake wazalendo walikuwa ni viongozi mashuhuri katika medani zote kwenye ngazi mbalimbali. Wanachama wengi wa TANU walikuwa wanawake na walihusika na majukumu ya kuchangisha fedha, uhamasishaji wa nyumba hadi nyumba na ushawishi wa wanachama katika makundi mbalimbali.”

Kitabu hiki ambacho mwandishi wake ni Susan Geiger, kimetafsiriwa na kurahisishwa na Elieshi lema kwa niaba ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TNGP), kwa lengo mahsusi kuwakumbusha Watanzania na wale wote wanaojali na kuheshimu utu, kutambua kuwa nafasi ya wanawake katika jamii haipaswi kudharauliwa, kubezwa na hata kukejeliwa kwa visingizio mbalimbali. Hili linapotendeka, huu ndio haswa, unyanyasaji kijinsia.

Kitabu hiki kilichosheheni visa mkasa lukuki kinaeleza kwa kina wanawake hawa wazalendo walivyojenga uelewa wa ni nini maana ya utaifa kunzia TANU.

Kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni ya chama cha Waandishi  wa Habari Wanawake Tanzania ( TAMWA  juu ya ujanyanyasaji wa kijinsia, hali bado ni mbaya. Hali hii ina maana gani kwa serikali, wanaharakati, wanahabari kadhalika Watanzania kwa jumla.

Hii inataka jitihada za ziada katika ngazi zote kuanzia serikali za mitaa hadi serikali kuu.    

 Mwaka 2011, nilisafiri kwa basi  toka kituo kikuu cha mabasi ya abiria yaendayo mikoani cha Ubungo jijini Dar es Salaam, kuelekea wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

Kama kawaida ya safari za mikoani, basi hilo likiwa limeenea abiria katika viti vyote, liliondoka katika kituo hicho saa 12.30 asubuhi.

Baada ya mwendo mathalani wa saa mbili, nakumbuka mama mwenye mtoto wa kike mwenye umri kama miaka mitano, alimfuata kondakta na kumweleza kuwa mtoto alihitaji kujisaidia.Kwa mujibu wa mama huyo  alijibiwa asubiri kidogo.

Nakumbuka vizuri kwamba basi lilipamba moto hadi tukafika sehemu ya kuongeza mafuta. Mama yule ambaye alilazimika kurudi katika kiti chake baada ya kuambiwa asubiri, alimjongelea tena dereva kumkumbusha nia yake ya kumpeleka mtoto ajisaidie.

Huwezi kuamini kwamba dereva alimkatalia yule mama na kuendelea kuchanja mbuga. Kilichofuatia ni ukulele mzito toka kwa kina mama waliokuwa ndani ya lile basi. Amini usiamini, dereva alilazimika kusimamisha basi na mama yule kumpeleka mwanaye nje ili ajisaidie.

Ukatili kama huu uleta kilema cha maisha.
Hii kama haitoshi, kina mama ndani ya basi lile kwa umoja wao, walimlaani dereva kadiri kila mmojawao alivyojaliwa na muumba wake. La kushangaza, kina baba walifumba midomo yao kana kwamba hawakusikia wala kuona kilichokuwa kikiendelea baina ya dereva ambaye ni mwanaume mwenzao na mama wa mtoto.

Niliwaza sana na kuwazua kuhusu hili, nikaogopa sana kuhusu maisha yetu iwapo katika kipindi hiki miaka zaidi ya hamsini tokea tujitawale bado tu kina baba hawana uchungu wa kuona kwamba mama awaye yeyote  ni sawa sawa na mama yako. Kadhalika,umwone mtoto wa mwenzio, jirani, rafiki kuwa ni mwanao.

Kutoka Sengerema, kurudi Dar es Salaam nikiwa katika basi tofauti na lile la awali, nilishuhudia kituko kingine kutoka kwa dereva wa basi hilo.

Baada ya mwendo wa karibu kutwa nzima. Majira kama ya saa nane au tisa mchana, aliruhusu abiria kuchimba dawa (kujisaidia) wakati yeye akiongeza mafuta katika basi. Lakini sehemu hiyo ilikuwa na choo chenye vyumba viwili tu. Kimoja kwa wanaume na kimoja kwa wanawake. Hilo kama halitoshi, ni sehemu ambayo mabasi mengi husimama kuongeza mafuta na abiria kuchimba dawa (kujisaidia).

Nakumbuka wakati huo kulikuwa na mabasi takribani matatu. Fikiria abiria wangapi walihitaji huduma hiyo kwa wakati mmoja. Kilichotokea ni kwamba, wanaume kwa jinsi Mungu alivyowajalia, waliweza kujificha ficha na hivyo kuwahi kwenye mabasi kabla ya wanawake.

Hali hiyo ilisababisha wanawake washindwe kujikamilisha kabla ya muda ambao ulitolewa. Dereva   wa basi nililopanda akaondoa basi bila ya kujali kuwa, kuna wanawake walikuwahawajaingia licha ya kuelezwa. Kama kawaida akapigiwa kelele na wasamaria wema na kutishiwa kuwa wangempiga laiti angewaacha kina mama hao.

Visa mkasa hivi viwili, ni vionjo tu nilivyokupa ndugu MTANZANIA. Katika kisa mkasa cha mwanzo, unaona wazi ni jinsi gani ukatili wa kijinsia unavyotesa wanawake. Mama huyu na mwanae wa kike wote wameangukia katika lindi la kufanyiwa ukatili.

MTANZANIA mwenzangu ni mara ngapi tumeshuhudia tukiwa safarini, wanaume wanavyowaomba madereva wasimame ili wajisaidie. Tena, kila wanapojisikia, wala hawajali kama ni mahali pa wazi au penye usiri.Tena wako baadhi ya madereva, wanaotumia fursa za wanaume kuwasimamisha  mara kwa mara, kuwapa pia  fursa hiyo abiria wengine, bila kujali kuwa sehemu husika haitawafaa wanawake. Huu ni UKATILI WA KIJINSIA.

Kisa mkasa cha pili, kadhalika. Ni wajibu wa madereva kuhakikisha kuwa sehemu wanazowapeleka abiria wao ‘kuchimba dawa’ zinakidhi mahitaji ya wanawake na wanaume kwa wakati mmoja?. Iwapo hazikidhi, basi watafute maeneo ambayo hayatakuwa ya  karaha hususan kwa wanawake na wasichana.

Jambo lingine kubwa na la msingi ni kwamba, mara nyingi wasafiri hawa huandamana na watu wanaowaheshimu. Ambao kwa mujibu wa tamaduni zetu, hawawezi wakaandamana nao ‘kuchimba dawa’ katika eneo moja. Lazima mmoja awe mbali na mwingine. Mfano, mama amesafiri na babake mzazi/baba mkwe. Au mtoto mwenye umri mkubwa amesafiri na mama yake mzazi/mama mkwe. Katika haya, WATANZANIA wenzangu tusidanganyane kwamba tunakwenda na wakati. Haya hayana wakati, tumezaliwa tumeyakuta na tutaendelea kuyaenzi kwa faida ya vizazi vijavyo.

 

Dominica Cassian Haule, ni Mwandishi wa Habari / Mchambuzi wa Masuala ya Jinsia   na Mwenyekiti wa Asasi ya Jinsia na Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania – GEMSAT.

dominicahaule@yahoo.com

 

 

 

   

UKATILI WA KIJINSIA

Na Dominica Cassian Haule

Ukatili wa kijinsia ni msemo mpana sana. Unagusa binadamu wote wanawake na wanaume. Lakini ni ukweli usiopingika kwamba ukatili wa kijinsia unawaathiri kwa asilimia kubwa wanawake na wasichana kuliko ilivyo kwa wanaume na wavulana. Kuna tafiti lukuki zinazothibitisha. Wakati wa mababu na mabibi zetu, tulisikia mwanamke kapigwa, kavunjwa mkono, kauawa na kadhalika na kadhalika. Tuliongozwa na tamaduni na kuona maisha ndivyo yanavyotakiwa kuwa.

URITHI Binafsi, nashawishika kuamini kuwa, ukatili wa kijinsia, umekuwepo tokea mwanzo wa uzao wa binadamu. Ukipitia maandiko mbali mbali, utakuta maandiko, mtu na mkewe. Kwa hili mimi na wewe hatuna budi kujiuliza, hivi mtu ni nani?  Lakini pia katika maandiko hay ohayo, utakutana na semi binadamu wote. Basi, na tubadilike, tukijua kuwa kwa kuwa neno binadamu wote inamaanisha watu, kwa hiyo, watu hao ni wanawake na wanaume.

Katika familia zetu, kilio kikubwa bado kinaumiza mabinti pale ambapo wazazi/walezi wanapogawa majukumu fulani kuwa ya wasichana na mengine kuwa ya wavulana. Mara nyingi inasahaulika kuwa, vyovyote iwavyo, majukumu ya wasichana yanaweza kuchukua asilimia kubwa ikilinganishwa na asilimia ya majukumu ya wavulana.

Japo kwa asilimia fulani, wakazi wa mijini wameweza kutambua umuhimu wa kuwapa watoto wao majukumu yanayofanana ili mradi hayavuki mipaka. Hii ni njia mojawapo ya kutoa malezi endelevu kwa watoto wote wa kike na wa kiume. Kadhalika tumeshuhudia, wazazi wanaojadili kutegemea uzao wa watoto wa kiume tu. Na haya yanapatiwa baraka na wanawake pia. Fikiria mama mjamzito anapolazimika kuomba ajaliwe mtoto wa kiume.

Lakini sio kwa matashi yake, bali kwa matashi ya jamii inayomzunguka. Imemtengenezea mtizamo wa kuthamini mtoto wa kiume japoku yeye ni mwanamke. HABARI SAHIHI Vyombo vya habari kwa ujumla wake navyo vinachangia kwa kasi kuwanyima uelewa mpana wananchi ili waachane na vitendo vinavyochangia ukatili wa kijinsia. Haviandiki au kutangaza kwa undani yale yanayopinga ukatili wa kijinsia, ili wananchi wapate upembuzi yakinifu. Kwa mujibu wa jarida, Jinsia na Vyombo vya Habari Tanzania, lililobeba stadi juu ya mwendelezo wa jinsia na vyombo vya habari (2010), sauti za wanawake zinasikika pale tu habari inapohusu ukatili wa kijinsia na usawa wa kijinsia. Ambazo zinachukua asilimia 71 na 67.

Na habari hizo ni zile za udhalilishaji, mfano ukahaba, mauaji ambayo yametendwa na mwanamke na kadhalika. Ingefurahisha na kupongezwa iwapo habari hizo zingekuwa zile zinazoleta maendeleo kwa nchi, ukizingatia kwamba asilimia 70 – 75 ya kazi za uzalishaji hasa sehemu za vijijini hufanywa na wanawake. La kusikitisha, habari zinazohusu madini kwa mujibu wa jarida hilo hazikupata nafasi katika vyombo vyetu vya habari. Sambamba na hizo, zile zinazohusu ajira zilipata fursa kwa asilimia kumi tu na zile zinazohusu makazi zilipatiwa nafasi kwa asilimia kumi kadhalika.

Stadi juu ya mwendelezo wa jinsia na vyombo vya habari Tanzania iliyoratibiwa na asasi isiyo ya kiserikali ya Jinsia na Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania – GEMSAT kwa ufadhili wa asasi isiyo ya kiserikali yenye makao makuu nchini Afrika kusini –‘ Gender Links’, imebaini pia kwamba asilimia sita (6) ya wanawake hubeba utambuzi wa mama, mke au binti kwa upande wa chanzo cha habari. Wakati asilimia nne tu (4) ya wanaume hubeba utambuzi wa baba, mtoto wa kiume au mume. Hili lina maana gani kwetu. Ni kwamba, mwanamke au msichana bado anatambuliwa kupitia kwa baba yake mazazi/mlezi au kupitia kwa mumewe.

Tanzania yenye raia wa kike na kiume
wenye furaha inawezekana
Japokuwa ukatili wa kijinsia umebainika kufanyika kwa kiwango cha kutisha si tu nchini Tanzania, bali hata katika nchini zilizopo kusimwa mwa Afrika, ni asilimia tatu tu (3) ya habari zinazoandikwa na kutangwa zinaongelea ukatili wa kijinsia. HISTORIA Kwa mujibu wa kitabu WANAWAKE WA TANU (Jinsia na Utamaduni katika Kujenga Uzalendo Tanganyika: 1955 – 1965),”wanawake wazalendo walikuwa ni viongozi mashuhuri katika medani zote kwenye ngazi mbalimbali.

Wanachama wengi wa TANU walikuwa wanawake na walihusika na majukumu ya kuchangisha fedha, uhamasishaji wa nyumba hadi nyumba na ushawishi wa wanachama katika makundi mbalimbali.” Kitabu hiki ambacho mwandishi wake ni Susan Geiger, kimetafsiriwa na kurahisishwa na Elieshi lema kwa niaba ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TNGP), kwa lengo mahsusi kuwakumbusha Watanzania na wale wote wanaojali na kuheshimu utu, kutambua kuwa nafasi ya wanawake katika jamii haipaswi kudharauliwa, kubezwa na hata kukejeliwa kwa visingizio mbalimbali. Hili linapotendeka, huu ndio haswa, unyanyasaji kijinsia. Kitabu hiki kilichosheheni visa mkasa lukuki kinaeleza kwa kina wanawake hawa wazalendo walivyojenga uelewa wa ni nini maana ya utaifa kunzia TANU.

Kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni ya chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania ( TAMWA juu ya ujanyanyasaji wa kijinsia, hali bado ni mbaya. Hali hii ina maana gani kwa serikali, wanaharakati, wanahabari kadhalika Watanzania kwa jumla. Hii inataka jitihada za ziada katika ngazi zote kuanzia serikali za mitaa hadi serikali kuu. Mwaka 2011, nilisafiri kwa basi toka kituo kikuu cha mabasi ya abiria yaendayo mikoani cha Ubungo jijini Dar es Salaam, kuelekea wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

Kama kawaida ya safari za mikoani, basi hilo likiwa limeenea abiria katika viti vyote, liliondoka katika kituo hicho saa 12.30 asubuhi. Baada ya mwendo mathalani wa saa mbili, nakumbuka mama mwenye mtoto wa kike mwenye umri kama miaka mitano, alimfuata kondakta na kumweleza kuwa mtoto alihitaji kujisaidia.Kwa mujibu wa mama huyo alijibiwa asubiri kidogo. Nakumbuka vizuri kwamba basi lilipamba moto hadi tukafika sehemu ya kuongeza mafuta. Mama yule ambaye alilazimika kurudi katika kiti chake baada ya kuambiwa asubiri, alimjongelea tena dereva kumkumbusha nia yake ya kumpeleka mtoto ajisaidie. Huwezi kuamini kwamba dereva alimkatalia yule mama na kuendelea kuchanja mbuga.

Kilichofuatia ni ukulele mzito toka kwa kina mama waliokuwa ndani ya lile basi. Amini usiamini, dereva alilazimika kusimamisha basi na mama yule kumpeleka mwanaye nje ili ajisaidie. Hii kama haitoshi, kina mama ndani ya basi lile kwa umoja wao, walimlaani dereva kadiri kila mmojawao alivyojaliwa na muumba wake. La kushangaza, kina baba walifumba midomo yao kana kwamba hawakusikia wala kuona kilichokuwa kikiendelea baina ya dereva ambaye ni mwanaume mwenzao na mama wa mtoto. Niliwaza sana na kuwazua kuhusu hili, nikaogopa sana kuhusu maisha yetu iwapo katika kipindi hiki miaka zaidi ya hamsini tokea tujitawale bado tu kina baba hawana uchungu wa kuona kwamba mama awaye yeyote ni sawa sawa na mama yako. Kadhalika,umwone mtoto wa mwenzio, jirani, rafiki kuwa ni mwanao. Kutoka Sengerema, kurudi Dar es Salaam nikiwa katika basi tofauti na lile la awali, nilishuhudia kituko kingine kutoka kwa dereva wa basi hilo.

Baada ya mwendo wa karibu kutwa nzima. Majira kama ya saa nane au tisa mchana, aliruhusu abiria kuchimba dawa (kujisaidia) wakati yeye akiongeza mafuta katika basi. Lakini sehemu hiyo ilikuwa na choo chenye vyumba viwili tu. Kimoja kwa wanaume na kimoja kwa wanawake. Hilo kama halitoshi, ni sehemu ambayo mabasi mengi husimama kuongeza mafuta na abiria kuchimba dawa (kujisaidia). Nakumbuka wakati huo kulikuwa na mabasi takribani matatu. Fikiria abiria wangapi walihitaji huduma hiyo kwa wakati mmoja. Kilichotokea ni kwamba, wanaume kwa jinsi Mungu alivyowajalia, waliweza kujificha ficha na hivyo kuwahi kwenye mabasi kabla ya wanawake.

Hali hiyo ilisababisha wanawake washindwe kujikamilisha kabla ya muda ambao ulitolewa. Dereva wa basi nililopanda akaondoa basi bila ya kujali kuwa, kuna wanawake walikuwahawajaingia licha ya kuelezwa. Kama kawaida akapigiwa kelele na wasamaria wema na kutishiwa kuwa wangempiga laiti angewaacha kina mama hao. Visa mkasa hivi viwili, ni vionjo tu nilivyokupa ndugu MTANZANIA. Katika kisa mkasa cha mwanzo, unaona wazi ni jinsi gani ukatili wa kijinsia unavyotesa wanawake.

Ukatili wa kupigana kati ya mke na mume
mara nyingi wanawake hudhurika zaidi.
Mama huyu na mwanae wa kike wote wameangukia katika lindi la kufanyiwa ukatili. MTANZANIA mwenzangu ni mara ngapi tumeshuhudia tukiwa safarini, wanaume wanavyowaomba madereva wasimame ili wajisaidie. Tena, kila wanapojisikia, wala hawajali kama ni mahali pa wazi au penye usiri.Tena wako baadhi ya madereva, wanaotumia fursa za wanaume kuwasimamisha mara kwa mara, kuwapa pia fursa hiyo abiria wengine, bila kujali kuwa sehemu husika haitawafaa wanawake. Huu ni UKATILI WA KIJINSIA.

Kisa mkasa cha pili, kadhalika. Ni wajibu wa madereva kuhakikisha kuwa sehemu wanazowapeleka abiria wao ‘kuchimba dawa’ zinakidhi mahitaji ya wanawake na wanaume kwa wakati mmoja?. Iwapo hazikidhi, basi watafute maeneo ambayo hayatakuwa ya karaha hususan kwa wanawake na wasichana. Jambo lingine kubwa na la msingi ni kwamba, mara nyingi wasafiri hawa huandamana na watu wanaowaheshimu. Ambao kwa mujibu wa tamaduni zetu, hawawezi wakaandamana nao ‘kuchimba dawa’ katika eneo moja. Lazima mmoja awe mbali na mwingine.

Mfano, mama amesafiri na babake mzazi/baba mkwe. Au mtoto mwenye umri mkubwa amesafiri na mama yake mzazi/mama mkwe. Katika haya, WATANZANIA wenzangu tusidanganyane kwamba tunakwenda na wakati. Haya hayana wakati, tumezaliwa tumeyakuta na tutaendelea kuyaenzi kwa faida ya vizazi vijavyo. Dominica Cassian Haule, ni Mwandishi wa Habari / Mchambuzi wa Masuala ya Jinsia na Mwenyekiti wa Asasi ya Jinsia na Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania – GEMSAT. dominicahaule@yahoo.com

Friday, September 26, 2014

Tanzania Women in Peace Networking-TAWOPE, congratulate the Constitutional Assembly on the Draft of New Constitutional, whereby a whole chapter for Land issues also inserted. This is first and last improvement on this new constitutional. TAWOPE have been fighting and empowering women to make sure that they also own land officially, inherit etc. Meanwhile our struggle won, we need to congratulate one another, either to strengthen on what we have been done. Huree!!! On 16th August, 2014 TAWOPE had a session with CA Members, and the main theme was to lobby them to make sure that Land issue is very contraversial and a source of conflict whereby we would like to be well recognised and considered. Now it is there, this hopes that even the UN Resolution 1325 will soon be ratified. Specifically I congratulate Dada Dominica Haule Kamugisha, she is the one went to Dodoma physically and sit together with some of the CA members. We also thank you the URGENT ACTION FUND for supporting our move.

Saturday, June 28, 2014

VYOMBO VYA HABARI VYA KIJAMII - Toeni elimu kwa jamii madhara ya unyanyasaji kijinsia Na Gladness Hemedi Munuo Vyombo vya habari vya kijamii (Community Media) vikitumika sawasawa katika kutoa habari vitajenga na kuwa msaada mkubwa wa maendeleo kwa jamii katika kuelimisha madhara yanayokuwa kwa kasi sana ambayo ni unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake, watoto na wazee. Zipo jamii nyingi sana Afrika na hususan Tanzania ambazo mila na desturi huwageuza wanawake kuwa ni viumbe duni visivyo na sauti na hata kutofaa kustahili kuwa na haki. Na wahanga wakubwa wa mila na desturi zenye mfumo dume ni wanawake na watoto ambao kukandamizwa kwao kunatafsiriwa kama ni jambo la kawaida kwa jamii. Mikataba mbalimbali ya kimataifa na kikanda ambayo nchi ya Tanzania kupitia bunge letu tukufu imeridhia, imeeleza kwa undani kuhusu uwajibikaji wa jamii na taifa kwa ujumla katika kuhakikisha kuwa mwanamke na mtoto analindwa na kuheshimiwa kama ilivyo kwa mwanaume. Hivi karibuni katika mkutano mkuu wa kwanza na kongamano kwa vyombo vya habari vya kijamii (Redio za jamii) uliofanyika mjini Bagamoyo, mambo mbalimbali yalijadiliwa katika kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vya kijamii vinaimarika na kuwa msaada muhimu kwa jamii iliyovizunguka hasa katika kuelimisha kuutoko,eza unyanyasaji. Naweza kusema kuwa, kwa jinsi kasi ya manyanyaso, uonevu na ukatili kwa wanawake na watoto unavyopamba moto siku hadi siku, wapo wataalamu mbalimbali waliotoa ari kuwa vyombo vya habari vya kijamii viwe ndiyo nguzo kubwa katika kutoa elimu kwa jamii, kwa kuwa mpaka sasa ndivyo vyombo vinavyofanya kazi kwa niaba ya jamii na karibu na jamii (Cabrella-Balleza,M.’Community media by and for women’;AMARC women’s International Network, 2007). Majadiliano hayo yalilenga katika kuona kuwa vyombo hivi ambavyo kwa ujumla takribani kwa idadi vipo zaidi ya vyombo 20 walihudhuria kongamano hilo, walitoa ari kwa vyombo hivyo viwe na manufaa kwa asilimia 100 kwa wana jamii, ikiwa ni msaada katika kuondoa kero zilizopo pamoja na kuelimisha na kuburudisha. Suala moja wapo lililowekewa mkazo ni kuhakikisha kuwa vipindi vyote vya redio viandaliwe katika mfumo wa kuhakikisha vinakidhi matakwa ya jamii zote na zaidi wanawake na watoto ili kwenda sawa na ‘Protokali ya Jinsia na Maendeleo katika kanda ya kusini mwa Afrika’. Ambayo katika kifungu cha 29-31kinazungumzia masuala ya habari, taarifa na mawasiliano na msisitizo ni kuwa ifikapo mwaka 2015 masuala ya jinsia katika vyombo vya habari yatakuwa yameshika kasi nzuri kutokana na mafunzo mbalimbali yanayotolewa kwa waandishi wa habari, aidha sera za jinsia zitaendelea kuwepo na kuhamasisha waandishi katika kutetea masuala ya jinsia. Sio jambo geni kwetu tunaposikia taarifa mbalimbali kupitia vyombo vya habari zikituhabarisha matukio ya unyanyasaji kwa wanawake na watoto yanavyokuwa siku hadi siku, na ndiyo maana msisitizo umetolewa katika kuhakikisha vyombo vya habari vya kijamii kuweka agenda ya mkakati wa kutoa elimu hii kwa umma. Katika kongamano la kwanza kwa vyombo vya habari vya kijamii, kero za unyanyasaji wa jinsia kwa jamii ilionekana kushika kasi hasa kutokana na takwimu sahihi kama zinavyoainishwa na ‘Tanzania Demographic and Health Survey (TDHS)’ ya mwaka 2010. TDHS inaonyesha kuwa unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto wa kike ambao hawana ndoa ni asilimia 44% wakati wanawake walio katika ndoa ni asilimia 20. Ikumbukwe kuwa hizi ni takwimu kwa matukio yaliyotolewa taarifa katika vituo vya polisi na mahospitalini, na penginewe ni sehemu za mijini tu. Kwa maana kwamba zipo taarifa nyingi za matukio kama hayo katika maeneo ya vijijini na zaidi ambazo hazijajulikana. Hii ni kutokana na wana familia na jamii kuamua kuyafumbia macho matatizo kama hayo na kuyageuza kama jambo la kawaida katika familia. Katika kuchangia mada hii, mwakilishi kutoka katika Redio ya Jamii Kigoma, alielezea masikitiko yake kuhusiana na haki ya watoto kielimu inavyoporomoka kiasi kusababisha watoto wa kike kukosa elimu kwa kupata ujauzito wakiwa mashuleni. Naye mshauri wa redio/vyombo vya habari vya kijamii kutoka UNESCO Bi Rose Haji alielezea umuhimu wa sera za jinsia na vyombo vya habari zinavyopaswa kufanyiwa kazi kwa vitendo, ikiwa ni pamoja na uandaaji wa vipindi, muda wa kurusha vipindi hewani kulingana na ratiba au desturi za kila siku za jamii husika. Jambo lililopongezwa katika kuhakikisha kuwa itakuwa ni rahisi kwa habari lengwa kufika kwa walengwa bila pingamizi, ni kuwepo kwa matumizi ya lugha ya Kiswahili ambayo mpaka sasa imani kubwa ni kuwa watanzania walio wengi lugha hii wanaifahamu na hasa kwa kusikia na kuelewa hata kama hawatazungumza. Hivyo basi, wito ulitolewa kwa wanahabari wa vyombo vya kijamii kutumia vyombo vya habari ikiwa pamoja na kalamu zao kama vitendea kazi katika kuhakikisha kuwa jamii inatambua madhara ya unyanyasaji yaliyopo kwa upande wa wanawake na watoto. Washiriki na wajumbe katika kongamano hilo walijadili kwa kina ya kuwa njia nzuri ya kufikisha ujumbe kwa walengwa (wasikilizaji) ni kuwepo kwa hatua za awali katika kuhakikisha hilo linatekelezeka kwa kuwajengea uwezo waandaaji na wapelekaji wa habari hizo kwa jamii kupitia vyombo vya habari vya jamii. Elimu kama hii imekuwa ikitolewa na asasi kama vile Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Asasi ya Jinsia na Maendeleo ya Vyombo vya Habari Tawi la Tanzania (GEMSAT), Baraza la Habari Tanzania (MCT) nchini na vimekuwa mara zote vikiwalenga zaidi waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya kawaida na kuwasahau waandishi waliopo katika vyombo vya habari vya kijamii. Kongamano hilo ambalo liliendeshwa kwa siku tatu, lilionyesha imani kubwa kuwa, vyombo vya habari vya kijamii vikiwezeshwa kisawasawa, basi litakuwa daraja muhimu katika kuirekebisha jamii au kuondoa kabisa kero za unyanyasaji wa kijinsia kwa jamii. Ukitaka kujua ni kwa vipi wanawake na watoto wananyanyasika kijinsia, tembelea katika vituo vya polisi vilivyopo katika maeneo ya makazi ya watu. Aidha pita katika hospitali na vituo vya afya upate kujionea visa mkasa na madhila yanawapata wanawake walio wengi. Aidha mila nyingi za jamii mbalimbali nchini Tanzania zinaongeza a na kuona kama ni sehemu ya maisha na mwanamke hana sauti ya kujitetea. Aidha, wapo wale wanaodhani kuwa, desturi ya ukandamizaji na uonevu kwa jinsia isiyo na sauti (wanawake) ni jambo sahihi au suala la kawaida. Wito umetolewa kwa wamiliki wa vyombo vya habari vya kijamii kuvalia njuga elimu ya kukomesha unyanyasaji kwa wanawake na watoto. Suala hili likitiliwa mkazo mafanikio yataonekana. Tushike maneno ambayo Hayati baba wa taifa hili muasisi wa serikali yetu na Rais wa kwanza wa Tanzania Mheshimiwa Julius Kambarage Nyerere, ambaye aliwahi kusema kuwa ‘inawezekana ikiwa kila mmoja atatimiza wajibu wake’. Gladness H. Munuo: Ni Mratibu wa Asasi ya GEMSAT Mobile No.+255 754 285701
TOGETHER WE CAN: Dar es Salaam hosts first SADC Gender Protocol Summit  Maternal Health project by CSSC became an overall winner Country and Regional wise By Gladness Hemedi Munuo Gender Links (GL) in Collaboration with Gender and Media Southern Africa Tanzania Network (GEMSAT) on March 27, 2013 hosted the first ever SADC Gender Protocol Summit at Dar es Salaam’s Blue Pearl Hotel in Tanzania. This Summit sought to comment and encourage local level initatives towards achieving the 28 targets of the SADC Gender and Development Protocol, which Tanzania has recentlry ratified. In her opening remarks, Deputy Minister for Community Development, Gender and Children, Ummy Mwalimu said that the Tanzania government aligns itself with SADC Gender and Development Protocol to achieve gender equality. Mwalimu assured stakeholders and participants that government will work closely with the media and civil society to promote gender equality in the country because ‘togethe we can’. The summit accompanied together with the provision of different Awards to various entrants to recognise the efforts made by organisations, media houses and journalists to push the gender agenda and create awareness about women’s issues and gender equality. With light blue sweater she is speaking with the community is Ms. Rache Mkunduai, a Public Relation Officer with CSSC trying to educated people on what is ‘Kangaroo Style’ and its advantages. As per this information, GEMSAT member of the Board congatulate Ms. Rachel Mkundai, Public Relations Officer of Christian Social Services Commission (CSSC) was commended and awarded in country and SADC Regional wise for the organisations contribution towards the achievement of gender equality through reproductive and maternal health “I am happy to have worked with GEMSAT and other organisations” she said so. A mother delivered premature in a Kangaroo Style of carering at one of the Health Center after CSSC introduced the practice.(All photos by CSSC) Rachel presented on a success story on how they educat3 majority rural area on how to care on premature babies by using ‘Kangaroo style’ and its success in most parties they intriduced in Tanzania. Therefore, CSSC has done such a recommendable job on that. All in all, the summit intends to mobilise media houses, journalists and civil society to unite and fight for gender equality. GL with GEMSAT is currently working with ten media houses in Tanzania, who have committed to mainstreaming gender in institutional practices and content. The summit awards rewarded journalists and media organisations who are at the forefront of gender reporting.
MIGOGORO NA VURUGU HUIBUA UNYANYASAJI KIJINSIA KWA WANAWAKE • Azimio la Umoja wa Mataifa no.1325 lilete mabadiliko Tanzania • Mabaraza ya Usalama kwa Vijiji, Kata, Wilaya na Mkoa washirikishe Wanawake Na Gladness Hemedi Munuo Imefika wakati wa nchi yetu Tanzania kupitia bunge letu tukufu kuridhia Azimio la Umoja wa Mataifa ya 1325 (UN Resolution 1325) ili kukomesha vitendo vya kikatili na unyanyasaji kijinsia wanavyotendewa wananchi wasiokuwa na hatia na hasa wanawake katika maeneo yenye migogoro. Hii ni kwa kuwa, nchi zote zilizo katika Umoja wa Afrika Mashariki tayari zilikwisha ridhia Azimio hili la Umoja wa Mataifa na utekelezaji wake ili kukidhi haja za jamii zao. Iweje Tanzania mpaka leo tunasusua wakati tayari migogoro, vita na mashambulizi ya aina mbalimbali kwa jamii hivi sasa yameshamiri. Uhalisia kamili umethibitisha kuwa, mahali popote panapotokea mgogoro, baina ya jamii kwa kutokuelewana kiasi cha kuzuka mapigano na uharibifu wa mali, vitendo vya unyanyasaji kijinsia vinavyojitokeza kama vile ubakaji kwa wanawake na watoto, utekaji nyara wa watoto wa kiume na wasichana ili waweze kuwatumikia watekaji kama watumwa au wake zao, pamoja na jamii hasa wanawake kuachwa wakiwa walemavu au kuharibiwa baadhi ya viungo vyao. Azimio la Umoja wa Mataifa la 1325, linapinga kuwepo kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha kuwa wanawake wanahusishwa katika ngazi zote za maamuzi kuhusiana na kupatikana kwa amani nchini na duniani. Vyombo vya habari vimekuwa vikijitahadi kuhabarisha umma kuhusu matukio dhalimu kama haya, lakini kwa uhakika wanao/walioathirika na majanga kama haya ni wengi, na kwa kuwa vyombo vya habari ni vichache vinavyoweza kufika vijijini na hasa maeneo yenye migogoro ili kuibua na kuhabarisha umma kikamilifu vitendo vya unyanyasaji kijinsia kwa jamii na hasa wanawake si rahisi habari nyingi kufika katika vyombo vya usalama kwa haraka. Upo msemo unaosema ‘wapiganapo tembo nyasi ndizo zinazoumia’, pamoja na ‘Vita vya Panzi ni furaha kwa Kunguru’. Misemo hii inaashiria kuwa, wakati wowote tusikiapo ya kuwa kuna mgogoro wa aina fulani kiasi kupelekea jamii kukimbia makazi yao, wazee na wagonjwa huachwa bila ya msaada wowote aidha, wapo wakina mama wanaojifungulia maporini maeneo ambayo hayana usalama kiafya ikiwa ni pamoja na wanawake kufanyiwa vitendo vya kikatili kama vile kubakwa, kulawitiwa nk. Hivyo basi, muarobaini wa athari hizi, ni kuwepo kwa maridhiano ya Azimio la Umoja wa Mataifa no.1325, ili utekelezaji wake uanze mara moja, huenda dawa ya kutokomeza migogoro hii ikiwa ni pamoja na kutibu itakuwa imekamilika kwa njia hii. Asasi ya Wanawake katika mapambano ya amani Tanzania (TAWOPE), ni moja wapo ya taasisi yenye malengo ya kuhakikisha kuwa, jamii na wanawake waliopo katika maeneo yenye migogoro wanapatiwa elimu mbalimbali kama vile kujilinda na jinsi ya kujikinga miili yao kufuatia kuzuka kwa migogoro na vurugu za mara kwa mara, ufahamu wa sheria ya ardhi vijijini ya mwaka 1999 na elimu nyingine mbalimbali. Mbali na TAWOPE, aidha zipo asasi ambazo zimejikita katika kutoa misaada mbalimbali kwa waathirika wa migogoro ya aina yeyote ile, ikiwa ni pamoja na ushauri nasaha kwa walioathirika kwa njia moja au nyingine, hizi ni asasi kama Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania (TAWLA), Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), na wengineo wengi. Aidha, zipo asasi zinazotakiwa kuwa mstari wa mbele katika kushughulikia waathirika wa migogoro hiyo kama vile waliobakwa na kupata majeraha, ujauzito na hata maradhi mbalimbali ikiwemo UKIMWI, hawa huhitajika kupata msaada wa kiafya kutoka asasi husika kama vile Chama cha Madaktari wa Kike Tanzania (MEWATA), pamoja na asasi zenye kutoa huduma kama hizo. Aidha, katika utafiti uliofanywa na TAWOPE (2010), ilionyesha kuwa katika nchi ya Tanzania maeneo ambayo kwa hakika migogoro isiyokwisha hujitokeza mara kwa mara, ni maeneo wanayoishi wafugaji na wakulima, na kikubwa hasa ni kwa wafugaji kuwa na idadi kubwa ya mifugo ambapo mara zote huingiza mifugo kwenye mashamba ya wakulima na kusababisha kuzua kutokuelewana kati yao na wakulima. Ingawaje maamuzi ya UN ya 1325 yanalenga kulinda na kutetea maslahi ya wanawake hasa katika maeneo ambayo migogoro au vurugu zenye matumizi ya silaha zimejitokeza upande mmoja au pande zote. Siyo siri kuwa, hata Tanzania, wananchi walio wengi wameshuhudia baadhi ya wafugaji wakitumia silaha ikiwa ni pamoja na bunduki zenye risasi za moto, ambazo madhara yake ni makubwa kwa jamii yote na hasa kwa wanawake ambao wamekuwa ndiyo kichaka cha uonevu. Je, mpaka leo tujiulize, Tanzania tunasubiri nini mpaka Azimio hili litupite? Vurugu au migogoro ya hivi karibuni jamii imeweza kushuhudia wakati wa Operesheni mbili za kitaifa (Tokomeza na Kimbunga), kumekuwa na vitendo vya ubakaji na kila aina ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wanaume waliokumbwa katika hizo operesheni ambazo ziligeuka na kuwa ni vurugu kwa jamii husika. Mfano halisi wa wanawake walioathirika ni pale ambapo baadhi yao wamelazimika kuolewa kinguvu na wafugaji au askari wanaosimamia operesheni mbalimbali kama tulivyoshuhudia nchini Tanzania hivi karibuni. Taarifa kama hizi zinasimuliwa na waathirika wenyewe katika maeneo ya Mahenge –Itete, Morogoro- Mvomero, Loliondo na Manyara. Aidha, Mara-Tarime, Pwani –Rufiji pamoja na maeneo mengine ambayo wafugaji wameingia kwa wingi. Angalizo pia tunatoa kwa serikali yetu, katika kipindi hiki ambacho wananchi wanajiandaa na uchaguzi wa taifa, zipo dalili ya kujitoza kwa vurugu za kisiasa ambazo kwa Tanzania tumeshashuhudia baadhi ya vifo mfano mauaji ya mwandisha wa habari huko Iringa, aidha vurugu za silaha za moto (bomu) kwa raia wasiokuwa na hatia katika nyumba za ibada Zanzibar na Arusha, na hata katika mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa.. Kipindi hiki Tanzania inapoandaa Katiba Mpya, ndiyo wakati muafaka wa kuhakikisha pia Azimio la Umoja wa Mataifa no.1325 linazingatiwa kwa kuridhia na kuhalalisha utekelezaji wake ili migogoro iliyopo na inayoendelea kujitokeza iweze kudhibitiwa. Hivyo basi, mapambano dhidi ya vitendo vya unyanyasaji kijinsia yanahitaji ushirikiano kutoka serikalini, asasi zote zenye kuunga mkono haki za binadamu pamoja na vyombo vya habari katika kuhabarisha jamii. • Mwandishi Gladness Munuo ni Mratibu wa Asasi ya Jinsia na Vyombo vya Habari, Tawi la Tanzania. 0754/0786/0754 285701